Mechi ya watani wa jadi Yanga na Simba imemalizika kwa sare ya goli moja kwa moja , Mechi hiyo iliopigwa katika dimba la taifa , Mchezo huo uliotawaliwa na ubabe, Mwamuzi Martin Sanya alimzawadia kadi nyekundu nahodha wa Simba Jonas Mkude baada ya nahoza huyo kumsukuma muamuzi wa pambano hilo kutokana na kutokua makini katika mchezo huo kwa kulikubali goli la yanga liliofungwa na mshambuliaji Hamisi tabwe dakika ya 27 kipindi cha kwanza baada ya kuunawa mpira huo kabla ya kuutumbukiza nyavuni mpira huo, Goli hilo lilipelekea mpira kusimama zaidi ya dakika saba baada ya mashabiki wa simba kuanza kung`oa viti na kuvitupa uwanjani . Vuruguhizo zilipelekea jeshi la polisi kutumia nguvu ya ziada kwa kufyatua mabomu ya machozi ili kuweka mambo sawa na baada yahali kuwa shwari mpira uliendelea na mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika yanga walitoka uwanjani wakiwakifua mbele kwa goli moja , Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa timu zote kufanya mashambulizi ya